ZOLENDRONIC

ZOLENDRONIC

23-05-2022

12:15

Story ya KITAPELI Wakati niko Advance ile likizo kabla ya mitihani ya utani (MOCK) nikarudi zangu home. Nikapewa hela za tuition nisome prac. nijiandae na paper Kuna jamaa yangu akaniomba nimkopeshe zile hela atanirudishia in one week period, with interest.

Nikaona ni BINGO, nika-buy in.. nikampa zote (km 70k hivi) kwa makubaliano kuwa atanirudishia 100k Jamaa akapotea mazima. Nikashindwa kusoma practical. Ile likizo inaisha nikaona kabsa kwa jinsi nlivyo mweupe nitaaibisha ukoo kwenye MOCK. Ikabidi nitengeneze plot nisifanye MOCK

Kuna siku nikarudi nyumbani nikawaambia naumwa mgongo, wakashtuka sana.. wakanipa hela nikapime pale Sekou Toure Nikaenda nikaonana na daktari akanambia sina shida kubwa ila natakiwa kupumzika tu Kweli mgongo ulikuwa unauma sometimes prolly sababu ya kukaa sana, PCB msuli tembo

Basi nikarudi home nikawaambia daktari amesema natakiwa kupumzika wiki 3 mifupa itulie ndo nikafanye kipimo😂😂 Wakanielewa, wakaulizia habari za shule na mtihani nikawahakikishia nitali-handle Baada ya km siku 5 shule ikafunguliwa

Mock ilikuwa a week baada ya kufungua Basi nikajituliza home under maximum supervision wakati wenzangu wana-dissect vyura huko😂😂 Mtihani ukapita, nikapata nafuu.. nikawashauri home waniruhusu nikamalize shule kabisa afu nirudi sasa nitibiwe kwa UTU na UTULIVU - wakanikubalia

Usafiri wa meli usiku, kule shuleni nmeingia asubuhi, kinyonge sana.. jioni yake nikaenda zangu fellowship nikapewa nafasi ya kuongea chochote Ikabidi nitafute sympathy yao kwanza.. nikasimama kinyonge sana ndani ya mjaketi mkubwa - nikasema nlikuwa naumwa sana

...ndio maana sikutokea hata kufanya MOCK Nikawaambia nimepima, japo majibu bado hayajatoka ila kuna uwezekano mkubwa ikawa KANSA ya mifupa au kitu kingine serious Wana wakasikitika sana, wakatangaza maombi ya siku 3 kumsihi Mungu kwa ajili yangu

Wakaanzisha mchango kunitia moyo, wakachanga km 28k pale pale Ile stori ya kansa ikasambaa shule nzima, mpaka staff kwa walimu. Wana kibao wakaomba 'kushow love' kunichangia kwa nia njema kunitia moyo. Basi kumbe walimu pia wakaji-organize.. wakatoa ten ten. Km 170k hivi

Nikaitwa ofisini kwa mkuu msaidizi, nikakabidhiwa mzigo. Ticha akanisihi sana nikate bima itanisaidia kupunguza gharama za matibabu. Nikamhakikishia kuwa hilo ni jambo jema, na nitalizingatia Shule ilikuwa na form 3 mpaka 6 (ilikuwa wakimaliza hao waiondoe O-level)

Baada ya wiki moja nikapata wito wa kufika ofisi ya kiongozi wa social upande wa wanafunzi - kiranja Nikatembea kinyonge sana nikisindikizwa na roommate kadhaa mpaka nikafika.. nikakuta mzigo km 220k wanafunzi wamejichanga shule nzima kunitia moyo na kusimama na mimi😎

Story ikafika mpaka church nlipokuwa nasali, wao pia wakaamua kumuaibisha shetani.. wakafanya changizo.. nikapata 130k Wakatangaza maombi ya siku 3 kusimama na mimi...

Matokeo ya MOCK yakatoka, kweli paper kimtindo ilikuwa ngumu maana kuna mwanangu mmoja Biology P1 alipata 1, P2 akapata 3. Jumla 4% Huyo mwana ni mtu mkubwa kwa sasa yuko huko Zambarau(ze fyucha ze papo)😂😂

Basi nikafurahi sana kwa sababu sijaaibisha ukoo na hela nimepata.. Mwaka wetu kulikuwaga na migomo ya hapa na pale so walimu wakasusia kutuandalia graduation. Tulivyomaliza NECTA nikawachukua wanangu wa PCB 7 tukashuka club moja maarufu pale mjini kujipongeza. hela si ipo?

Ile nmerudi home nikakutana na yule mwamba aliyenipiga hela za Prac. Ile ameniona tu akanivuta kwa wakala akatoa 110k fasta akanikabidhi.. nikaona maisha nmeyapatia Baada ya wiki 2 akanitafuta tena akanambia kwa sababu this time niko free anishirikishe dili tupige hela

Nikamkubalia ila nikamuomba apige tu mwenyewe mi anigawie faida.. Akanambia mtaji ni km 1.5M ila tukipata 1M tunaanza.. basi nikampa hela zangu zote za KANSA (km 430k hivi). Nikabaki na ile 110k aliyonilipa..

Bahati mbaya yule mwamba this time alinizima kikweli kweli kabisa.. sikupata hata sent'ano ya ile biashara Moral of the story Ukitaka kula, nawe lazima uliweFollow us on Twitter

to be informed of the latest developments and updates!


You can easily use to @tivitikothread bot for create more readable thread!
Donate 💲

You can keep this app free of charge by supporting 😊

for server charges...