WatuNiStory

WatuNiStory

05-06-2022

14:35

"Nina miaka 25 nipo Kigoma. Nilikuwa na mahusiano na mdada mmoja hivi, tangu mwezi wa tisa mwaka 2016 kipindi hicho yeye alikua mwanafunzi so sikutaka kuharibu malengo yake sikuwahi kumuuliza wala kumtaka kimwili mpaka akamaliza shule ndio tukakutana 2017.

Kuanzia hapo tulipendana sana mpaka tukatambulishana home yaani mahusiano yetu mpaka wazazi walikua wanafahamu. Ilikuwa furaha kwakweli.

Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka akaenda chuo Tabora na mimi nikabaki Kigoma nikiendelea na mishe mishe za utafutaji huku tukiwasiliana kwenye simu kila siku. Kiukweli nilimjali sana, nilimtumia hela ya matumizi kila mwezi, kila kiti kilichokuwa ndani ya uwezo wangu, nilimpa

Sikutaka akose chochote, hata wazazi wake walipopungukiwa kwenye ada, mimi niliongezea pale wazee walipopungukiwa. Hiyo ikafanya kwao wanipende mno. Nilitoa msaada kwao na mtoto pia. Shida ilikuja 2020, alipata ujauzito. Kiukweli hakutaka kwao wafahamu.

Tuliweka siri mpaka akajifungua ndio tukafikisha taarifa nyumbani. Kwa bahati nzuri alijifungua mwezi wa kwanza baada ya kuhitimu chuo. Kwao walikua wakali ila badae walielewa wakatulia. Nikampa mtoto jina la mama yangu. Maisha yakaendelea na kwao waliamini nitamuoa.

Kwa bahati mbaya miezi miwili badae Mama yangu alifaliki so mambo yakazidi kuwa magumu kwangu. Nikajikuta naahilisha suala la ndoa na yule binti ili nikae sawa. Tukakubaliana tusogoze mbele suala la ndoa Ili tujipange vizuri.

Badae wakati mimi ndio nakamilisha mambo yangu taratibu akaanza kubadilika akawa ananifanyia visa ilimradi tuachene tu. Suala la ndoa akawa halitaki tena. Kiukweli mara kadhaa niliwahusisha ndugu zake ila wakawa wananipa tu moyo wakasema mimi ndio mkwe wao hakuna mwingine.

Mtoto akatimiza mwaka. Yule mwanamke akiwa bado hataki kufunga ndoa na mimi. Mwanaume niliendelea kumhudumia mtoto, nilimpenda sana mwanangu. Atake nini nisimpe? jina lake lilinikumbusha marehemu mama yangu.

Sasa ikawa tunasumbua sana kwenye masuala ya hela, yaani kila mwezi nilikuwa natuma pesa ya matumizi na siku za sikukuu mwanangu hakosi nguo mpya. Ilikua natuma pesa mpaka muda mwingine nilihisi ananikomoa. Ila sikutaka kujali sana maana nilijua natuma kwa ajili ya mtoto wangu.

Sasa kimbembe kimekuja hivi majuzi, kuna jamaa nilikuta amepost picha za mwanangu huku akijisifu amekuza. Nilishangaa, kiukweli nilihisi kama naota.

Ikabidi nimfuatilie jamaa mpaka nikapata namba yake, nikampigia akaniambia ukweli kwamba yeye yupo Tabora na alikutana na huyu mdada huko chuo na kumbe walikua wana mahusiano tangu 2020 na ndio alimpa mimba.

Ilinibidi nimuulize mhusika mwenyewe (mama wa mtoto) akakiri ni kweli akaniambia na mtoto sio wangu ni wa huyu jamaa wa Tabora yaani hapo nilitamani hata kufa kwani nilipoteza muda na gharama nyingi kwa ajili ya mtoto.

Niliwaambia wazazi wake, kumbe mama yake alikuwa anajua ila aliogopa kuniambia. Baba yake tu ndo alifichwa. Sasa baba yake yeye hataki mwanamke aolewe kwingine anataka mimi ndio nimuoe. Hata mahali hataki, yaani ameniambia nikachukue mke bureee.

Sasa mimi nachoomba unifikishie kwa wadau wanipe ushauri , nikaoe huyu mwanamke nilee mtoto asie wangu au niachane nae niendelee na maisha yangu? Please usiache kufikisha ujumbe huu". Anonymous, Kigoma. #WatuNiStoryFollow us on Twitter

to be informed of the latest developments and updates!


You can easily use to @tivitikothread bot for create more readable thread!
Donate 💲

You can keep this app free of charge by supporting 😊

for server charges...